Sala kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 18 wa Shirika la Neno la Mungu

2241831695_2612348c0a_z(2)

Sala kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 18 wa Shirika la Neno la Mungu

Ee Mungu Utatu Mtakatifu,
Baba, Mwana na Roho,
tunakushukuru kwa zawadi ya Shirika la Neno la Mungu
na ya wito wetu wa kimisionari.
Tunnakutuza kwa ajili ya Moyo Safi wa Mwanao Yesu,
chemichemi ya huruma na neema.

Wakati sisi Wamisionari wa neno la Mungu
tunapojiandaa kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa kumi na nane,
washa ndani yetu moto wa pendo lako.
tusaidie kufanya upya utashi wetu
ili tuwe kila wakati tumezama katika Neno wako
kama chanzo na msingi wa maisha, wito na utume wetu.

Upendo wako usio na mipaka utufanye
kuwa wanafunzi wamisionari wanaobadilisha
kwa kuhubiri Ufalme wako wa amani na uwiano,
katika kila pahali, kati ya watu wote na tamaduni zote.
Kwa kila chochote tufanyacho,
pamoja na wadau wetu katika utume,
tulifanye hili kwa upendo wa kweli kama ulivyotupenda wewe.

Maria, mama wa Neno la Mungu, utuombee
ili tufuate nyayo zako
na kuimarika katika utashi wetu kwa Mwanao.
Kupitia kwa maombezi ya Mt. Arnold Janssen na Yosefu,
Wabarikiwa Maria Helena na Yosefa,
na mashahidi wetu,
tunaomba ili Moyo wa Yesu
uishi ndani ya mioyo yetu na mioyo ya watu wote.

 

Fr.  Lawrence Muthee SVD

2 thoughts on “Sala kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 18 wa Shirika la Neno la Mungu

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Blog at WordPress.com.

Up ↑

%d bloggers like this: