Mwenyeheri Gregorius Frackowiak, SVD.

Nyamwaya copyWatakatifu ni watu ambao waliishi maisha yao kwa kutenda matendo ya kawaida kwa njia isiyo ya kawaida. Maisha yao na mafunzo yao yanavutia wengine kuiga mwenendo wao. Watakatifu wana uhusiano wa karibu sana na wafia dini,  ambao ni watu  waliotoa maisha yao hadi kufa kwa ajili ya kutetea Imani katika Dini zao. Hawa hujitolea kuteseka hadi kufa kwa kushuhudia imani yao.

Mfano mzuri ni ule wa Mwenye Heri Gregorious Frackowiak ambaye alizaliwa katika familia ya watoto kumi na wawili, katika kijiji cha Boleslaw Frackowiak katika Mji wa Lowecice karibu na Poznan. Wazazi wake walimlea katika mazingira ya kikristu. Alijiunga na Shirika la Neno la Mungu akiwa na umri wa miaka kumi na nne (14). Alitamani kwa dhati kuwa Bruda. Alipokelewa na kuanza malezi ya Novishiati Gorna Grupa. Baada ya Novishiati alifanya kazi katika mapokezi ya maktaba ya vitabu, na baada ya kuzuka vita vya pili vya dunia; Mwenye heri Gregorious  alikuwa mmoja wa wale walioteswa na kufa kwaajili ya kutetea imani zao. Hii ni baada ya Gorna Grupa kufanywa kituo cha mateso ya Mapadre.

Mtakatifu Gregorious aliyaacha makazi yake Gorna Grupa  alipokua akifanya kazi,  na kwenda kufanya kazi sehemu mbalimbali kama vile, Parokia ya Mtakatifu Martin kama mhudumu wa Sakristia na pia kuwafundisha watoto imani ya Kanisa Katoliki. Baadae alijiunga na wachapisha Jarida la Jaricin, lililokua likichapisha habari za kupinga  wapiganiji wa Nazi waliokua  wanapigana katika vita ya pili vya dunia. Wapiganaji hao walipogundua uwepo wa  kikundi hiki waliwakamata na kuwafunga Gerezani, walikotesa hadi kufa.

Mwenye heri Gregorius alijitolea kufa kama mfia dini na kifo chake kinaweza kikalinganishwa na kile cha Mtakatifu Maximilian Maria Kolbe aliyekufa kwa kukatwa kichwa  tarehe 05, Mei 1943; akiwa na miaka thelathini na mmoja ( 31) tu.

Mtakatifu Maximilian Maria Kolbe alikua kijana wa umri mdogo zaidi akilinganishwa  na wafia dini wenzake watatu wa shirika la Neno la Mungu. Alifia Gereza liitwalo Dresden. Ili kuonyesha kufa kwake ni kujitolea kama mfia dini, aliwaandikia familia na marafiki zake barua hii:

“Ninawaandikia barua hii kwa mara ya mwisho katika dunia hii, mtakapoipokea barua hii sitokua tena katika dunia hii. Siku ya Jumatano ya tarehe 05, Mei1943; Saa 12:15 Jioni nitanyongwa. Sasa limebaki lisali moja tu Padre aniletee Mwili wa Kristo. nawasihi mniombee ili Roho yangu ipumzike kwa Amani Mbinguni. Nawaachia yote, kama mkipenda mwaweza kumjulisha Mama yangu juu ya kifo changu. Nimepumzika kwa Amani. Nawasalimu ninyi nyote, na nawangoja wote mbele za Mungu. Tafadhali wasalimu Wamisionari wote wa Ndugu Bruczko na baada ya vita naomba mpeleke Kanzu yangu hapo. Mungu awabariki mbaki waaminifu katika Kanisa Katoliki. Naomba msamaha wa makosa yangu yote. Namhurumia sana Mama yangu. Mungu awabariki.  Tutaonana Mbinguni .”

 

By Frt.  Nyamwaya George Okong’o

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Blog at WordPress.com.

Up ↑

%d bloggers like this: