MAANA WIKI KUU

Wiki Kuu ni wiki ya sita ya kipindi cha kwaresma ambayo uanza Dominika ya Matawi hadi Jumamosi Kuu katika liturjia ya Kirumi.

  1. Jumapili ya Matawi – Tunaadhimisha siku ambayo Yesu aliingia Yerusalemu wazi na kama mfalme. Kabla ya siku hii, Yesu alienda Yerusalemu mara kwa mara kama wayahudi wengine hasa wakati wa Pasaka. Mara hii, Yesu anaingia Yerusalemu mara ya mwisho kwa sababu hatarudi tena Galilaya akiwa hai. Anaingia akiwa tayari kuutoa uhai wake kwa ajili ya dhambi zetu (Mt 21:1-11)
  2. Alhamisi Kuu – Siku hii tunaadhimisha siku ambayo Yesu alikula karamu ya mwisho na wanafunzi wake. Katika siku hii Yesu alitangaza wazi kwamba saa yake ya kuteswa na kufa ilikuwa imewadia. Hivyo, Yesu aliweka alama ambazo zimedumu katika Kanisa hadi leo. Nazo ni:
    1. Sakramenti ya Ekaristi – Yesu alitoa mkate na divai na kuvibariki kama ishara na mfano wake kati ya wanafunzi wake na kuwaamuru kufanya hivyo mara kwa mara kwa ukumbusho wake (Lk 22:7-23)
    1. Sakramenti ya Upadrisho – Yesu aliwaamuru wanafunzi wake kuadhimisha mwili na damu yake ili kudumisha uwepo wake nao katika Jumuiya. “fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu” (Lk 22:19). Kwa mjibu wa Upadrisho wake, Padre ni umwilisho wake Kristu.
    1. Amri ya Utumisho kwa Upendo – Kwa kuwaosha miguu wanafunzi wake angali yeye mwalimu na kiongozi wao, Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuwatumikia watu kwa unyenyekevu na sio kupenda kutumikiwa.
    1. Ushirika – Katika karamu ya mwisho, Yesu aliweka alama ya umoja na kuacha viashiria vya umoja ambao ni upendo, kuumega mkate pamoja na kutumikiana (Yh 13:8-10)
  3. Ijumaa Kuu – Hii ndiyo siku ambayo Yesu alikamatwa, kushtakiwa kwa madai ya uongo na wayahudi kwa mamlaka ya Kirumi, na kuhukumiwa kifo. Yesu aliteswa na kudhihakiwa sana kabla ya kutundikwa msalabani na kufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu.
  4. Jumamosi Kuu – Usiku wa Jumamosi Kuu tunaadhimisha ufufuko wa yesu kutoka kaburini. Ufufuko wa Yesu ndio sababu ya uwepo wetu leo hii kama Wakristu. Kwa kufufuka yesu alishinda mauti na kuleta wokovu duniani. Mtume Paulo anatukumbusha kwamba, “Kama Kristu hakufufuka katika wafu, basi Imani yetu ni kitu bure” (1 Cor 15:14). Usiku huu tunaimba utukufu wa Mungu kwa kumfufua mwanawe Yesu kwa ajili ya kushinda mauti ya milele, adhabu iliyowekewa mwanadamu mdhambi.
  5. Jumapili ya Pasaka – Siku hii tunaamkia habari njema kwamba Yesu aliyeteswa na kuawa msalabani sasa amefufuka. Yesu alijidhihirisha kwa wanafunzi wake na sio watesi na wauaji wake. Aliwapa wanafunzi kazi ngumu ya kutangaza ufufuko wake. Yesu hakutaka kuwatisha watesi wake kwa kuwatokea akiwa hai, bali alitaka habari ya ufufuko wake iwafikie kwa mahubiri ya wanafunzi wake. Huu ni mtihani mgumu kwa wote ambao wangependa kuwa wafuasi wake. Haitakuwa tena kwa ushuhuda wa macho na milango mingine ya ufahamu ya mwanadamu bali kwa Imani katika mahubiri ya mitume na wanafunzi wake
  6. Leo hii wewe na mimi tu wakristu kwa sababu tumepokea na kuamini habari njema ya ufufuko wa wokovu tuliopokea kutoka kwa mitume na wafuazi wake Kristu kwa vizazi na vizazi
  7. Ni wito na jukumu letu sasa kumtangaza Kristu mfufuka kwa wale wanaotuzunguka kwa mananeno na matendo yetu ya Imani.

Fr. Lawrence Muthee, SVD

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Blog at WordPress.com.

Up ↑

%d bloggers like this: